Mshambulizi wa klabu ya Yanga Fiston Kalala Mayele bado ameonesha nia ya kuendelea kupambania ushindi hadi mwisho ufahamike nani ataibuka na Taji la Kombe la Shirikisho Barani Afrika CAFCC katika Fainali mchezo wa marudiano kati ya klabu yake hio au USM Alger
Wakiwa wanafanya maandalizi ya mwishoni, Mayele amesema kwamba imewabidi wasahau waliyopoteza nyuma cha muhimu ni kuto kata tamaa, na wanaamini kuwa watapata ushindi ugenini.
Yanga ilipoteza katika Mchezo wa kwanza wa Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika CAFCC wakiwa ndio wenyeji dhidi ya Timu ya USM Alger kutokea nchini Algeria ambayo wanatarajia kwenda kukutana nayo ikiwa katika ardhi ya Nyumbani.
Nyota huyo ndio alikipatia kikosi chake goli moja la kufutia machozi kabla ya mechi hio kutamatika kwa goli 1-2 USM Alger