Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Gianni Infantino ameipongeza Klabu ya Young Africans kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2022/2023.
Katika salama zake za pongezi alizoandika kupitia kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia alisema, isingekuwa rahisi kutwaa ubingwa huo bila bidii ya timu nzima, ari na kujitolea, na kila mtu kwenye klabu anaweza kujivunia hilo na akatoa pongezi kwa wote waliohusika katika mafanikio hayo.
Aidha Infantino ameipongeza TFF kwa mchango wake katika maendeleo na ustawi wa soka la Tanzania na Afrika.