Watoto wanaocheza densi wakiunda kundi linafahamika kwa jina la ‘Ghetto Kids’ kutokea nchini Uganda wamefanikiwa kutinga fainali ya shindano maarufu la uhalisia la vipaji, Britain’s Got Talent.
Ghetto Kids walishangiliwa kwa namna ya kipekee na waliofika kutazama mashindano hayo moja kwa moja pamoja na majaji wote wanne kufuatia onyesho lao la kusisimua lililoonyeshwa Jumatano usiku.
Kufuatia maonyesho hayo, waandaji Ant na Dec walizungumza na majaji na Alesha Dixon na Simon Cowell wakapendekeza kuchagua Ghetto Kids kama mchezo wao kuwa ni bora.
Watoto hao sita wenye umri wa miaka mitano hadi 13 ni yatima wanaoishi pamoja nchini Uganda baada ya kuasiliwa na baba yao Daouda Kavuma.
Sita hao ni miongoni mwa 31 ambao Daouda amewapa makao baada ya kuwapata wakiishi kwenye mitaa hatari ya jiji.
Wanatumia densi kuonyesha uwezo wao na kutimiza ndoto zao maishani.
Fainali ya mashindano ya Britain ya Got Talent itafanyika Jumapili, 4 Juni.
Cc; BBC Swahili
Congratulations Ghetto Kids!! You've just made it through to Sunday night's GRAND FINALE! 🥳#BGT #BGT2023 #BritainsGotTalent pic.twitter.com/4LldnP1fUr
— BGT (@BGT) May 31, 2023