Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) iliyo chini ya Wizara ya Katiba imetangaza matokeo kuhusu uchunguzi wa kifo cha Mwanafunzi wa UDOM, Nusura Hassan Abdallah ambayo yanaonesha kuwa kifo hicho hakina uhusiano wowote na ajali ya gari aina ya Toyota Land Cruiser V8 iliyomhusisha Naibu Waziri Dkt. Festo John Dugange usiku wa April 26, 2023 eneo la Iyumbu, Dodoma.
Tume hiyo imefafanua kuwa kifo cha Nusura kilitokea baada ya kuzidiwa akiwa nyumbani kwa mchumba wake anayeitwa Juma Mohamed Kundya, Mjini Moshi alikokwenda kwa ajili ya kupanga siku ya rasmi ya mchumba wake kwenda kujitambulisha nyumbani kwao Singida.
Aidha taarifa imeeleza kuwa Nusura alipelekwa Hospitali ya Faraja na baadae kufariki ambapo vipimo vilivyofanywa na Hospitali hio vilionesha kuwa kifo chake kilisababishwa na shambulio kali la kupanda kwa sukari na upungufu wa damu.
“Tume haikuweza kuthibitisha Mtu wa aina yeyote kuhusika na kifo cha Nusura kutokana na vielelezo vya Hospitali ya Faraja, Mkemia Mkuu wa Serikali, maelezo ya mengine ya Mashahidi, Daktari aliyempatia huduma na Ndugu wa Marehemu walioutayarisha mwili kwa ajili ya mazishi na kuuona mwili huo kabla ya mazishi walithibitisha kuwa haukuwa na dalili za kupigwa, kujeruhiwa wala majeraha” “Gari iliyopata ajali ilikuwa ni gari binafsi aina ya Toyota Land Cruiser GXR V8 yenye namba za Usajili T454 DWV iliyokuwa ikiendeshwa na Dugange na alikuwa peke yake katika gari hilo” ….., Imeeleza taarifa kupitia Tume hio #KoncepttvUpdates