Mkurugenzi wa Wasafi Media Naseeb Abdul @diamondplatnumz ametimiza ahadi yake ya kumkabidhi zawadi mlinda mlango wa klabu ya Yanga Djigui Diarra @djiguidiarraofficial.
Diamond alitoa ahadi hiyo wakati klabu ya Yanga ikichuana na ASM Alger katika mchezo wa fainali ya kombe la Shirikisho ambapo katika mchezo huo Golikipa huyo aliondoka na Tuzo ya Mchezaji bora wa Mechi Diamond amemkabidhi kipa Diarra kiasi cha Dola za kimarekani 4200 sawa na zaidi ya milioni 10 za Tanzania