Klabu ya Simba imewahi fikia hatua ya kushiriki Fainali ya CAF takribani miaka 30 iliyopita ambapo Mwameja Mohamed alikuwa nahodha wa kikosi cha timu hio.
Rais wa Jamuri ya Muungano Tanzania Mh Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweza weka bayana kuhusu ushiriki wa klabu hio katika michuano hio inayohusisha vilabu vilivyokuwa nafasi za juu katika Ligi Kuu ya Taifa husika.
Katika hafla ya Kuwapongeza Yanga kwa hatua waliofikia katika Michuano ya CAF msimu huu wa 2023 Ikulu Jijini Dar es Salaam ambapo Rais Samia aliialika Timu hiyo katika chakula cha Jioni na Kufurahia kwa pamoja hatua hio amesema…. “Simba wamewahi kucheza Fainali CAF 1993”.
Mwameja ndiye aliyewaongoza wachezaji wenzake wa Simba SC kuingia Uwanja wa Taifa (Benjamin Mkapa/ Lupaso) Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la CAF dhidi ya AS Aviação ya Angola mnamo mwaka 1993.
Simba ilishinda goli 3-1 ikiwa mwenyeji wa mchezo na kwa upande wa mchezo wa ugenini ilitoa sare ya 0-0 hivyo ikafuzu kwenda Fainali ambako ilifungwa 2-0 na Stella Club d’Adjamé ya Ivory Coast hapo hapo Uhuru baada ya kutoka na sare ya 0-0 Abidjan.
