Meneja wa Habari na Mawasiliano Simba SC Ahmed Ally ameendelea kusambaza ujumbe kupitia ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Twitter kuhusu klabu hio kuwa ilishawahi kucheza Fainali ya CAF Mwaka 1993, hakuna wa kuibeza kwani historia imeshawekwa kwa klabu hio kwakuwa haitofutika.
“Tulicheza Fainali ya CAF 1993 itabaki kuwa hivyo, Tanzania hii sisi ndo wa kwanza kucheza Fainali ya CAF. Huwezi kufuta historia hii hata ufanyaje labda dunia ianze upya yaan Adam na Hawa waje waanzishe upya uzao wa dunia.
Tunawashangaa wale wanaotumia nguvu kubwa kufuta historia hii, kama 93 ulikua hujui mpira hiyo haiondoi ukweli kuwa sisi tumecheza fainali Shida ni pale wanapotaka kuonekana wao ndo wa kwanza kufanya makubwa
Nchi hii kumbe wakulungwa tushafanya hivyo miaka 30 iliyopita Lakini pamoja na ukweli huo kuwa sisi tumecheza Fainali ya CAF, Hiyo ni historia yetu iliyopita, Sasa tunatakiwa kuandika Historia ya wakati huu 1993 ni Historia ya Mohammed Mwameja tunahitaji sasa
Historia ya Aish Manula Tunahitaji Kapombe aandike historia yake, tunahitaji historia itakayomuhusu Mohammed Hussein Tshabalala Kizazi cha mashabiki wa Simba wa 93 wanajivunia kuona Simba ikicheza Fainali, ni wakati sasa kizazi cha mashabiki wa sasa kushudia Simba yao ikicheza Fainali kwenye miaka yao Historia ipo kwa ajili ya kutonesha tulipotoka na tunapoelekea Tumeshajua tulipotoka sasa tuandae tunapoelekea”-Ahmed Ally, Meneja Habari na Mawasiliano Simba SC.