Msanii wa maarufu kutokea nchini Nigeria Davido amepakia (retweet) ujumbe uliambatanishwa na picha ya-screenshot iliyopo kwenye ukurasa mwingine unaofahamika kama “DAVIDO NEWS” kuonyesha namna video ya wimbo wake wa “UNAVAILABLE” aliomshirikisha Musa Keys umeweza tazamwa na Wafuasi wengi kwa kipindi kifupi tangu aipandishe ngoma hio kupitia akaunti yake ya YouTube.
Wimbo huo uliachiliwa rasmi April 11, Mwaka huu hadi kufikia mwezi huu karibuni imefikisha jumla ya Watazamaji (Viewers) Milioni 20 na zaidi.
Msanii huyu ameonekana kufurahishwa na mwitikio huo kutoka kwa Mashabiki zake na ndio maana ameamua kudhihirisha hisia zake katika hilo akiongezea kwa kuandika ‘FEEL @30’ kwa namna ya kipekee kusema hivyo kunaonyesha anataka kusema anahisi kama amefikisha Wtazamaji Mil. 30 sasa.
FEEL @ 30 https://t.co/A2hQAB3qO8
— Davido (@davido) June 4, 2023