Serikali ya Tanzania inapanga kujenga daraja la kilomita 50, refu zaidi barani Afrika kati ya Dar es Salaam na kisiwa cha Zanzibar.
Naibu waziri wa uchukuzi Mhandisi Geofrey Kasekenya, anasema mazungumzo yanaendelea na kampuni ya China Overseas Engineering Group (COEG), kampuni tanzu ya China Railway Group, ili kujenga daraja hilo.
“Tumekutana na wawekezaji watarajiwa wa COEG, na wameonesha nia ya kujenga daraja.” Aliongeza kuwa mazungumzo kuhusu mradi huo yalianza Machi na yalikuwa katika hatua ya juu.” Construct Africa imeripoti.
Serikali imekadiria daraja hilo lingegharimu $2.7bn kujenga, na inakusudia kufanya kazi hiyo kupitia ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi, huku baadhi ya fedha zikitolewa na benki ya maendeleo ya Afrika.