Uongozi wa Klabu ya Yanga umethibitisha kupokea Ofa kutoka Azam FC ikiwa na nia ya kutaka Kumsajili Mchezaji Feisal Salum kutokea klabu hio.
Baada ya Mazungumzo ya pande zote mbili na kwa kuzingatia matakwa ya kimkataba kati ya klabu na Mchezaji, Uongozi wa Young Africans Sports Club umefikia uamuzi wa kumuuza Mchezaji huyo kwa Klabu ya Azam FC
Mchezaji Feisal Salum ameuzwa kwenda Azam FC kwa dau ambalo halijawekwa wazi kutokana na makubaliano ya pande zote mbili.
Feisal ataungana na Timu yake mpya baada ya makubaliano binafsi na dirisha la usajili kufunguliwa rasmi.
Uomgozi wa Yanga SC umemtakia kila la kheri Feisali Salum katika majukumu yake mapya.