Josef Zinnbauer ndiye kocha mkuu mpya wa Raja Club Athletic, akichukua nafasi ya Mondher Kebaier ambaye alishindwa kufanikisha kufuzu kwa timu hiyo kwenye kampeni ya Ligi ya Mabingwa ya CAF msimu ujao.
Mtaalamu huyo wa Ujerumani hapo awali aliiongoza Orlando Pirates kati ya 2019-2021.
Josef (53) amesaini mkataba wa miaka miwili na kusema hivi baadaye:
“Nina furaha kuwa hapa Raja, najua klabu, najua jiji, najua wafuasi, nilikuwa na uzoefu dhidi yao. Lengo ni kushinda mataji hapa na kuleta mafanikio haraka iwezekanavyo.”(Micky Jnr).
#KoncepttvUpdates