Meneja wa Habari na Mawasiliano Simba SC Ahmed Ally amefunguka kuwa Mchezaji wa klabu hio (Saido Ntibazonkiza) aliyekuwa akichuana vikali na Mchezaji wa timu pinzani (Yanga) ndiye anastahili kutwaa tuzo ya Kiatu cha Mfungaji bora wa msimu huu.
Aidha alianza kwa kurejerea Vigezo vivyotumika kwa nmna timu zinazoshiriki Michuano ya Soka Barani Ulaya kwa wachezaji wanavyoshinda aina hiyo ya tuzo kwa kuwa mchezaji bora anavyostahili awe na kumalizia kwa kusema kwa takwimu hizo mchezaji wa Simba ndio anastahili kutwaa tuzo ya mchezaji bora.
“Mwaka 2012 kwenye mashindano ya UEFA EURO CHAMPIONS LEAGUE Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Hispania Fernando Torres alitwaa tuzo ya mchezaji bora licha ya kuwa na idadi sawa ya magoli na mshambuliaji Mario Gomez wa Ujerumani
Kigezo kilichotumika kumpa Torres kiatu cha dhahabu ni kuwa alicheza dakika chache kulinganisha na Gomes na pia Torres alikua na assist moja wakati Gomes hakua nayo
Fiston Mayele amecheza mechi nyingi 26 amefunga magoli 17 na Saidoo amecheza mechi chache 23 amefunga 17 na Asisst kama zote 12
Kwa mantiki hiyo Saidoo ndo mfungaji bora msimu huu kwani kama angecheza mechi sawa na Mayele angekua na magoli mengi zaidi” Ahmed Ally -Meneja Habari na Mawasiliano Simba SC