Mpishi wa Nigeria ambaye amekuwa maarufu nchini baada ya kupika bila kukoma kwa zaidi ya saa 93 amethibitishwa kuwa mshikilizi mpya wa rekodi ya dunia.
Wanasiasa na watu mashuhuri walimshangilia Hilda Baci jikoni kwake huko Lagos wakati wa kipindi cha siku nne mwezi uliopita.
Alitumia zaidi ya sahani 100 katika mchakato huo na aliruhusiwa tu kuchukua mapumziko ya dakika tano kila saa.
Baci amemshinda mshikilizi wa zamani wa rekodi Lata Tondon wa India, ambaye alisimamia muda wa saa 87 dakika 45 mwaka wa 2019.
Cc; BBC Swahili
The Guinness Book of World Records, ambao walilitoa uamuzi wa shindano la kupikia za Baci, wameshiriki video hii wakimpongeza:
After reviewing all the footage, we're delighted to announce that Hilda Baci is the new record holder for the longest cooking marathon (individual) 💫
Watch the video to find out the official time we've awarded Hilda and read the full explanation below 👇 pic.twitter.com/bf352ndxWO
— Guinness World Records (@GWR) June 13, 2023