Afisa habari wa Azam FC Hashim Ibwe amethibitisha kuwa Klabu hio imeachana tayari na nyota wake watatu waliokuwa wana mchango mkubwa ndani ya kikosi cha Azam ikiwa ni sehemu ya Maboresho ya Kikosi na wengine kutaka kupata changamoto mpya katika kucheza soka kwao.
Ametaja kuwa Listi ya Wachezaji hao kwa majina ni; Bruce Kangwa, Rodgers Kola na Keneth Muguna, Pia na sehemu ya makocha wao wanapungua.
Amesema kupitia Dirisha la usajili mpya ni Feisal Salum pekee ndiyo mchezaji anayehesabika katika Ingizo jipya la Usajili.
Amemalizia kwa kusema Bosi amechafukwa Mashine nne mpya zinatarajiwa kutua ndani ya Kikosi cha Azam pindi usajili tu ukifunguliwa, hii ni sehemu ya maboresho ya kikosi kwaajili ya michuano ijayo, kwahiyo usajili unaokuja kama timu itajipanga kutambulisha mashine kali mpya ili Azam iweze fikia Malengo iliyojiwekea.