Uongozi wa Klabu ya Yanga umeujuza umma kuwa umefikia makubaliano rasmi ya kuachana na kocha wao Nasreddine Nabi baada ya Kocha huyo kuomba kutoongeza mkataba mpya.
Mkataba wa Kocha Nabi katika kuitumikia klabu hiyo ya Wanajangwani umemalizika msimu huu.
Baada ya kumalizika mkataba huo Uongozi wa Yanga uliketi kuzungumza nae ili kuweza ona namna ya kumuongezea mkataba mpya lakini Kocha Nabi aliomba kuondoka kwenda kupata changamoto nyingine.
Kipindi yupo anahudumu ndani ya Timu ya Yanga katika nafasi yake ya Kocha Mkuu ameifanikishia klabu kutwaa ubingwa kwa Misimu Miwili na kuifikisha Timu katika hatua ya Fainali Michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika, CAFCC.
Kwa mchango huo mkubwa Kalbu ya Yangahaikusita kutoa pongezi za dhati kabisa kwa Kocha huyo kwani ameiandikia klabu hio historia mpya tangu kuanzishwa kwake mwaka 1935 na kuongezea kwa kumtakia kheri katika majukumu yake mapya huko aendako.
Klabu ya Yanga imeeleza kuwa imeanza mchakato wa kumtafuta Kocha mpya wa kuziba nafasi hio.