Waziri wa Fedha na Mipango Dk Mwigulu Nchemba amependekeza bungeni serikali kuanzisha mfumo wa kidijitali wa kufuatilia na kuhakikisha kodi husika za Serikali zinalipwa kwa wakati ikijumuisha matangazo ya Biashara ambayo huwekwa na Wahamasishaji wa Mitandaoni (digital influencers) na biashara za mtandaoni zinazofanyika hapa nchini.
“Kutokana na ukuaji wa teknolojia, Dunia inashuhudia mabadiliko makubwa katika tasnia ya matangazo ya kibiashara (Advertisement) ambapo sasa matangazo mengi yamekua yakifanyika kupitia mitandao (online advertisement) hasa mitandao ya kijamii kama vile Instagram, Facebook, twiter na Blogs mbalimbali.
Kwa kushirikiana na Sekta binafsi, Serikali inatarajia kuanzisha mfumo wa kidijitali wa kufuatilia na kuhakikisha kodi husika za Serikali zinalipwa kwa wakati. Hii itajumuisha matangazo ya Biashara ambayo huwekwa na watu maarufu (digital influencers) na biashara za mtandaoni zinazofanyika nchini,” amesema.