Poland inasema ubaguzi wa rangi haukuwa sababu ya uamuzi wake wa kuwazuilia walinzi wa rais wa Afrika Kusini na waandishi wa habari kwa zaidi ya saa 24.
Mzozo huo ulitokea katika uwanja wa ndege wa Chopin wa Warsaw. Ndege hiyo sasa itahifadhiwa hapo hadi Jumapili, msemaji wa uwanja wa ndege aliambia BBC.
Takriban watu 120 walikuwa wamekwama kwenye ndege hiyo, ambao ilikuwa ikielekea kwenye mkutano wa kilele wa amani nchini Ukraine.
Baadhi ya abiria sasa wanashuka na kwenda hotelini. Hatua za Poland zimemwacha Rais Cyril Ramaphosa, ambaye alisafiri kivyake kwenda Ukraine, bila baadhi ya maafisa wake wa ulinzi.
Hatua hiyo ilizua hisia kali kutoka kwa mkuu wa kikosi cha ulinzi wa Bw Ramaphosa, Meja Jenerali Wally Rhoode. “Wanatuchelewesha, wanaweka maisha ya rais wetu hatarini,” aliwaambia waandishi wa habari
“Tungelikuwa Kyiv kwa sasa lakini hivi ndivyo walivyoamua kutufanyia. Nataka muone jinsi walivyo wabaguzi.” Lakini Poland imepuuzilia mbali madai hayo.
CC; BBC Swahili