Uongozi wa Klabu ya Simba Umeitambulisha rasmi Kampuni ya Sandaland kuwa ndio mdhamini mkuu mpya (Msambazaji) wa jezi baada ya kumaliza mkataba na Vunjabei ambayo ilikuwepo katika nafasi hio ya udhamini kabla.
Sandaland ni kampuni inayojihusisha na uuzaji wa Mavazi mbalimbali ikiwemo Mavazi ya kimichezo (Sports Wear) kama sehemu ya Biashara yao kuu.
Kwasasa Sandaland ndiye anachukua jukumu rasmi la kuzalisha na kusambaza jezi kama ilivyokuwa kwa makampuni mengine hapo awali.
Simba SC inajivunia hatua kubwa iliyoweza kuifikia kwa kupata mapato mazuri kila hatua wanayozidi songa ndani ya klabu hio, Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu hio Imani Kajula amethibitisha kuhusiana na hilo;
“Nampongeza Sandaland kwa kupata nafasi hii, alijaribu mara ya kwanza hakufanikiwa lakini muda huu amepata. Namshukuru pia VunjaBei kwa udhamini aliotupatia.”
“Tunajipanga kusajili timu yenye ubora na usajili unakwenda vizuri. Simba inakwenda kuondoa unyonge, Simba ijayo.”- Mwenyekiti wa Bodi, Salim Muhene.“Sisi tunakuwa wa kwanza kwenye matukio makubwa na matukio muhimu na leo inakwenda kuwa hivyo.”- Ahmed Ally.