Baada ya Timu ya Taifa ya Tanzania alimaarufu kama “Taifa Stars” kuibuka na Ushindi wa Goli 1-0 dhidi ya Niger katika mchezo wa Kufuzu Michuano ya AFCON 2023 imejitengenezea nafasi nzuri ya kuweza pita katika Kundi iliyopo kwani hadi sasa imeshafikisha Pointi 7 ikiziacha Niger na Uganda chini yake.
Goli pekee lililofungwa na Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania Simon Msuva mnamo dakika ya 70′ ndilo limerejesha matumaini ya kufuzu michuano hio maana kwa mara ya mwisho timu hio ilipoteza katika mchezo wake dhidi ya Uganda na kusalia na chembe ndogo ya imani kuweza fanikisha kufika hatua hio japo ni mchezo huwa hautabiriki kwa fikra au mitazamo ya nje ya uwanja.
Taifa Stars inahitaji kushinda mechi moja itakayofuata ili kuweza fanikisha kabisa yake ya kufuzu AFCON 2023.
Baada ya Ushindi wa jana FT: TANZANIA 1-0 NIGER 70’— Msuva Msimamo,
Msimamo Kundi F
1. Algeria — 15
2. Tanzania — 07
3. Uganda — 04
4. Niger — 02