Mbunge wa Zamani wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi “SUGU” kupitia ukurasa wa Twitter amefunguka kuwa Dar inapendelewa sana wakati hata Mikoani nako kuna fursa zinazofanana.
Hiyo ni kufuatia Wanafunzi wa Kada ya Udaktari kutoka Sudan wamepewa nafasi ya kumalizia mwaka wao wa mwisho wa Masomo katika Hospitali ya Muhimbili iliyopo jijini Dar es Salaam kwake ahisi kama ni upendeleo kwa jiji hilo la Dar, na kwanini wasipelekwe hata mkoani kama Mbeya ambapo Hospitali kubwa kabisa ya Rufaa ipo pia
Ameandika “Haya mambo kila kitu inapendelewa Dar tuu ndio tunayakataa kila siku… Hata Mbeya ipo hospitali tena kubwa kabisa ya Rufaa, so nako wanafunzi hawa wangeletwa hata 10 tu…’ #TAITA- Joseph Mbilinyi, -Mbunge wa Zamani wa Mbeya Mjini
Haya mambo kila kitu inapendelewa Dar tuu ndio tunayakataa kila siku… Hata Mbeya ipo hospitali tena kubwa kabisa ya Rufaa, so nako wanafunzi hawa wangeletwa hata 10 tu… 😊😊 #TAITA pic.twitter.com/Uxs5v2HIkL
— Joseph Mbilinyi (@TheRealJongwe) June 20, 2023