Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, TFF linawakumbusha wanafamilia wa Mpira wa Miguu kuwa ni Kosa kushirikiana na wadau ambao wamefungiwa.
Ikielezwa kuwa ni muhimu kuzingatia kuwa wadau husika wamefungiwa baada ya kwenda kinyume na katiba, kanuni na taratibu zinazosimamia mpira wa niguu.
Hivyo, TFF inaendelea kufuatilia ukiukwaji huo ili kuchukua hatua stahiki.
Aidha imeelezwa kuwa, Wanafanilia wote wanao wajibu wa kuheshimu katiba, kanuni na taratibu za mpira wa miguu.
Pia waliofungiwa wanajiweka katika hatari ya kuchukuliwa hatua za kinidhamu iwapo hawatatumikia adhabu zao kikamilifu