Wanafunzi 150 wa udaktari kutoka Chuo Kikuu cha Tiba, Sayansi na Teknolojia (UMST) cha Khartoum nchini Sudan wamehamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ili kukamilisha mwaka wao wa mwisho wa masomo, kutokana machafuko ya kisiasa nchini mwao yaliyosababisha vyuo kufungwa.
Hayo yameelezwa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Prof Mohammed Janabi baada ya kuwapoke Wanafunzi hao kutokea nchini Sudan katika zoezi zima la kutaka wasaidia kukamilisha mwaka wao wa masomo hapa nchini.
Nchi ya Sudan imekumbwa na Machafuko ya Kisiasa kwa muda sasa hadi kupelekea kukwamisha utendaji katika shughuli nyingi za kijamii kama utoaji wa elimu na mengineyo ambapo inasababisha mambo mengi kukwama.