WATU Watano akiwemo Mtoto wa Kike mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 8 wamepoteza maisha huku wengine wakijeruhiwa baada ya Basi la Kampuni ya New Force linalofanya safari zake kati ya Dar es Salaam kwenda mkoani Rukwa kupata ajali katika Kijiji cha Igando kata ya Luguda Wanging’ombe, mkoani Njombe.
Kamanda wa Polisi mkoa huo, John Makuri Imori, amesema ajali hiyo imetokea hii leo Juni 21, 2023, majira ya Saa 8:30 mchana, baada ya dereva wa basi hilo kutaka kulipita (OVERTAKE) gari lingine bila kuchukua tahadhari na kupelekea kupoteza mwelekeo hadi kutumbukia kwenye mtaro.
“Taarifa za awali ni kwamba basi hilo lilikuwa linatoka Dar es Salaam, dereva alitaka ku-overtake lori likapoteza ueleko na kugonga daraja na kuingia mtaraoni, waliofariki mpaka sasa ni wanaume wanne na mtoto mmoja anayekadiriwa kuwa na miaka nane,” amesema Kamanda Imori