Mtangazaji wa Zamani wa Kipindi cha XXL ya Clouds FM amerejea katika kituo hicho cha kurusha matangazo baada ya kuhudumu kwa muda katika nafasi yake mpya akiwa E- Media inayohusisha E Fm na TV E chini ya Mkurugenzi mtendaji Francis Ciza (Majizzo).
B Dozen alijizolea umaarufu mkubwa kupitia namna ya Utangazaji na Ushawishi kwa Vijana wengi akiwa katika Kituo hicho cha Clouds Media.
Alikuwa miongoni wa watangazaji waliofanya muunganiko (Chemistry) kati yake na watangazaji wengine kama Adam Mchomvu, Mammy Baby kuonekana wenye ladha ya kipekee hasa kwa upande wa vijana wengi waliopenda kufuatilia kipindi alichokuwa anahusika pia.
B Dozen aliweza anzisha Chaneli ya Mtandaoni (Online Media) inayotumia jina lake hilo maarufu ikihusisha zaidi mahojiano na watu maarufu hasahasa wasanii wa muziki.