Huenda Msanii kutokea kipande cha Bongo Madee Seneda akaachana kabisa kujihusisha na Sanaa ya Muziki kufuatia kauli yake aliyoitoa kwa Maandishi kupitia ukurasa wa Mtandao wa Kijamii wa Twitter.
Kwa wasanii wa Kariba yake haijazoeleka kuona wanatembelea Kiki kuu-promote mziki wao maana hapa kutakuwa na Swali ni kweli yupo serious ama ndio ameingika katika mfumo wa kutembelea Kiki katika sanaa yake
Madee Seneda ameonekana kufunguka hivyo kwa hisia sana, ameanza kwa kumshukuru Mungu kwa nafasi aliyopewa kufikia umri aliyo nao ilihali wengine walishapoteza maisha kabla ya kufikia miaka hata 40.
Aidha amesema anasikitika kuwa kwanini amechelewa kuwa mtu mwingine, akiongezea kuwa umaarufu ni mbaya sana hivyo ameamua kuacha yote, na kuaanza kwa kusema “hataki tena Mziki” na mengineyo.
“Umri wangu umekwenda sana,na namshukuru Mungu kwa huu muda alionipa,coz nimeshuhudia marafik wengi sana hawakubahatika kufika 40+,why me?asante Mungu,nnachosikitika nikuchelewa kua mtu mwengine, Umaarufu mbaya sana,nmeamua kuacha yote,naanza nahili STAKI TENA MZIKI na mengineyo” ameandika Madee
Umri wangu umekwenda sana,na namshukuru Mungu kwa huu muda alionipa,coz nimeshuhudia marafik wengi sana hawakubahatika kufika 40+,why me?asante Mungu,nnachosikitika nikuchelewa kua mtu mwengine,
Umaarufu mbaya sana,nmeamua kuacha yote,naanza nahili STAKI TENA MZIKI na mengineyo🙏 pic.twitter.com/AzYQwOB1X4— Madee (@Madeeseneda) June 22, 2023