Idadi ya waliofariki kwenye ajali ya basi la Kampuni ya New Force iliyotokea Juni 21 mwaka huu, katika Kijiji cha Igando mkoani Njombe imefikia watu saba na majeruhi 48.
Kamanda wa Polisi mkoani humo, John Makuri Imori amesema wanaume waliofariki ni watano akiwemo dereva wa basi na wanawake wawili, huku akieleza chanzo cha ajali hiyo ni dereva kujaribu kulipita lori bila ya kuchukua tahadhari.