Mabaki ya mwili wa Christome Simon aliyekuwa mkazi wa mtaa wa Kambitano kata ya Lukobe, manispaa ya Morogoro ambaye alipotea tangu mwezi Novemba 2022, yamekutwa katika msitu wa Mgulu wa Ndege uliopo katika mtaa huo.
Kaka wa marehemu Joachim Simon, amesema ndugu yake alipotea katika mazingira ya kutatanisha kwani mara ya mwisho alionekana katika mtaa huo akiwa amevaa begi baada ya hapo hakupatikana tena, licha ya kupiga simu yake na kumtafuta maeneo mbalimbali na hakuwa na ugomvi wala migogoro na mtu yeyote.
Cc; JAMBO TV