Mwanafunzi wa kidato Cha tano katika shule ya Sekondori ya Panda hill, Ester Noah, amepatikana baada ya kupotea tangu Mei 18 ambapo zimepita zaidi zaidi ya siku 20.
Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, ACP Benjamini Kuzaga amesema Mwanafunzi huyo amepatikana majira ya saa tano asubuhi maeneo ya Ifisi katika Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mbalizi akiwa nyumbani kwa Azurath Abdul Mfanyabiashara wa genge katika maeneo hayo.
ACP Kuzaga amesema Azurath ameeleza kwamba mtoto huyo alimpokea kutoka kwa kijana muuza mkaa ambaye amekua akimuuzia magunia ya mkaa na kumuomba aishi naye kwa siku mbili wakati akitafuta chumba ili aweze kuishi na mtoto huyo. Itakumbukwa kwamba mwanafunzi Ester Noah alipotea May 18 akiwa shuleni Panda Hill.