Klabu ya Namungo FC ” The Southern Killers” Imethibitisha kumsajili Mchezaji wa zamani wa Simba SC, Erasto Nyoni ambaye aliagwa rasmi Alhamisi ya Juni 22 Mwaka huu.
Erasto Nyoni ni miongoni mwa Wachezaji wenye kariba ya Kucheza namba nyingi awapo uwanjani inategemea tu na Kocha anavyoamua kumpa aina ya majuku fulani ayafanye.
Kwa klabu yake ya Zamani “Simba SC” anatambulika kama Mchezaji “Kilaka” kulingana na uwezo wake huo wa kubadili namba za uchezaji apewapo au kukiwa na jukumu jipya linalomhitaji.
#WelcomeTosouthernkillersâś…
“Tunayofuraha kuwataarifu kuwa Erasto Edward Nyoni amejiunga kuitumikia Timu yetu ya Namungo Fc akitokea Simba Sc.
Karibu kwenye Familia ya Wauwaji wa Kusini Erasto Edward Nyoni” ….Imeandikwa na Namungo FC #southenkillers”Â