Aidha Rais Dk. Mwinyi amemueleza Balozi hiyo kuwa amepokea taarifa ya ujio wa Waziri wa mambo ya nchi za nje wa India na anamkaribisha sana Zanzibar.
Naye, Balozi Biyana Pradhan alimueleza Rais Dk.Mwinyi kuwa itaongeza maeneo mapya ya ushirikiano ni muhimu katika kuimarisha ushirikiano kati ya India na Zanzibar, pia ameahidi kuyashauri na kushawishi makampuni ya biashara ya utalii kutoka India kuingia Zanzibar.