Klabu ya Young Africans imemtangaza Kocha, Miguel Angel Gamondi kuwa Kocha wao mpya. Anakuja kuziba nafasi iliyoachwa na Kocha mkuu wa Zamani wa Klabu hio Nabi ambaye alimaliza mkataba wake na hakutaka kuongeza ili aweze kuhudumu zaidi.
Kocha huyo raia wa Argentina amewahi kuvinoa vvilabu kadhaa vya soka Barani Afrika kama Raja Casablanca ya Morocco, Esparance ya Tunisia na Mamelodi Sundowns kutokea Afrika Kusini.