Mwanamuziki kutokea nchini Nigeria, Damini Ogulu, a.k.a Burnaboy ameshinda tuzo ya Best International Act katika toleo la 2023 la Tuzo za Black Entertainment, BET.
Mwimbaji huyo wa ‘African Giant’ aliwashinda mastaa Ayra Starr, Central Cee na Stormzy, miongoni mwa wengine waliowania kinyang’anyilo hicho zaidi cha tuzo za BET.
Ingawa Burna Boy alikuwa kwenye onyesho hilo alipotangazwa kuwa mshindi, mama yake, Bose Ogulu, alipokea tuzo hiyo kwa niaba yake.
Bunaboy amekuwa akishangaza ndani ya miaka hii michache.
Albamu yake ya 2022 ‘Love, Damini’ ilifanikiwa kupenya ulimwenguni kote, na tayari alitwaa Tuzo ya BET katika kinyang’anyilo sawa mnamo 2019 na 2021.
Wengine walioteuliwa katika kinyang’anyilo hicho ni pamoja na Aya Nakamura, Ayra Starr, Central Cee, Ella Mai, K.O, L7nnon, Stormzy, Tiakola na Uncle Waffles.