Meneja wa Habari na Mawasiliano Simba SC Ahmed Ally kupitia Simba TV ametangaza kuwa Simba SC imeistaafisha jezi nambari 20 iliyokuwa inatumiwa na Kiungo wao Jonas Mkude hadi pale atakapopatikana mtu mwingine sahihi kutokea Simba B atakayeirithi ikiwa Mkude ameondoka Simba SC baada ya kuitumikia Club hiyo kwa miaka 13.
“Sisi kama Simba tumepanga kumfanyia makubwa sana Mkude katika kumuaga kwake, akimaliza mipango yake ya kimaisha ya kucheza ball arudi Simba SC nafasi yake kwenye utawala au ufundi nafasi yake ipo wazi” Ahmed Ally -Meneja Habari na Mawasiliano Simba SC
“La pili jezi namba 20 ambayo ameivaa Mkude kwa miaka 13 akiwa Simba SC nayo rasmi tumeistafisha haitatumika mpaka pale Simba tutakapopata kijana mwingine hodari kutokea Simba B” Ahmed Ally