Kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano Ofisi ya Rais Ikulu imeripotiwa kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dk. Samia Suluhu Hassan amefanya utenguzi na uteuzi wa nafasi za ukuu wa Wilaya (DC’s) kama ifuatavyo
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Mobhare Holmes Matinyi Kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Holmes amechukua nafasi hio baada ya kuwa Rais ametengua Uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mwanahamisi Munkunda
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua James Wilbert Kaji Kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mjini