Afisa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Yanga Ally Kamwe kupitia mkutano na waandishi wa habari amefunguka kuhusu nini kinachoendelea ndani ya klabu hio hadi sasa.
“Tumepokea mwaliko maalumu kutoka kwa Serikali ya Malawi kucheza mchezo maalumu kwenye maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru wa Malawi itakayofanyika Julai 6, 2023. Ni heshima kubwa sana kwa Klabu yetu na kwa Taifa kwa ujumla” Afisa Habari Young Africans SC Ally Kamwe
“Mgeni wa heshima kwenye sikukuu za uhuru wa Malawi ni Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na serikali ya Malawi ikatupa heshima hii ya kipekee kwa mualiko huu mkubwa na wa kihistoria” Ally Kamwe
“Napenda kutoa shukrani na pongezi kwa wachezaji wetu ambao watatoka mapumzikoni na kuungana nasi kwenda kuiwakilisha Nchi na Klabu yetu kwenye mualiko huu mkubwa. Tunatarajia kuondoka siku ya Jumatano na kama kawaida yetu ndege maalum kabisa itatupeleka Malawi na kutusubiri kisha tutarejea Dar es Salaam siku ya Alhamisi baada ya sherehe hizo” Ally Kamwe