Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imasaini mkataba wa makubaliano na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kupitia Mfuko wa Utamaduni na Sanaa utakaoiwezesha benki hiyo kutoa mikopo yenye ribaa nafuu kwa wasanii pamoja na kazi za sanaa na utamaduni hapa nchini.
Kwa mujibu wa mkataba huo, wasanii wataweza kukopa hadi shilingi milioni mia moja.
Riba katika mikopo itakayotolewa chini ya utaratibu huo itakuwa ni asilimia 9 tu. Mikopo itakuwa ikitolewa kwa hadi kipindi cha hadi miaka miwili.
Mkataba huo unaeleza kuwa, wasanii wataweza kupata mikopo ya ina mbili, kwanza mikopo kwa ajili ya uwekezaji na pili mikopo kwa ajili ya uendeshaji wa
shughuli zao za kibiashara.
Mikopo ya uwekezaji itawawezesha wasanii kukununua vifaa pamoja na kupata mitaji.
Mkopo huu utawawezesha wasanii kuwa na vifaa vya kisasa katika kazi zao na hivyo kupanua wigo wa biashara zao. Mikopo ya uendeshaji itasaidia
kuwapatia fedha zinazohitajika katika shughuli zao za kibiashara za kila siku.
Pamoja na mikopo hiyo ya riba nafuu, NBC itatoa elimu ya biashara na fedha kupitia Club za NBC Biashara. Elimu itakayotolewa itawasaidia kutoa ujuzi wa
namna ya kutunza fedha na pia kufanya maamuzi sahihi wanapotaka kuwekeza.
Huduma nyingine watakazonufaika nazo wasanii ni pamoja na bima aina mbali mbali, fursa za masoko na ushauri wa kifedha.
Akiongea wakati wa utiaji sahihi, mkurugenzi wa biashara wa NBC Elvis Ndunguru alisema “Benki ya NBC inayofuraha kuunganana na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuwawezesha wasanii wetu kupitia mikopo na elimu.
Mkataba huu ni mwanzo wa kuliwezesha kundi hili muhimu ambalo kwa kipindi kirefu liliachwa nyuma kwenye huduma za kifedha na mikopo. Kwa kuwapatia
mikopo yenye riba nafuu pamoja na elimu ya fedha, tutakuwa tumewasaidia kupiga hatua kiuchumi na kuendeleza sekta ya sanaa na utamaduni kwa upana
wake,” alisema.Mgeni rasmi katika hafla hiyo Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Pindi Chana aliishukuru benki ya NBC kwa kukubali kutoa mikopo kwa wasanii na
kusema kuwa hatua hiyo itasaidia kukuza sekta ya sanaa na utamaduni hapa nchini.
“Kwa niaba na Serikali, napenda kuishukuru sana benki ya NBC. Kupitia mkataba huu wasanii wetu hawatapata tena shinda ya mitaji kwa ajili ya kuendeshea
shughuli zao na pia wataweza kukuza biasahara zao,” alisema
Waziri alisema mtandao mpana wa matawi wa benki ya NBC ulioenea nchi nzima utawezesha wasanii kunufaika na huduma hii ya mikopo na elimu popote pale
walipo.
Ushirikiano huu kati ya NBC na Wizara, ni sehemu ya mkakati wa benki ya NBC kusaidia ukuaji wa uchumi wa nchi kupitia huduma za kifedha kwa kuyafikia
makundi mbali mbali na kuyapatia huduma kulingana na mahitaji yao mahususi.
MWISHO…………….