Klabu ya Young Africans SC rasmi imepokea Hundi yenye thamani ya TZS 405,000,000/= kutoka kwa mdhamini wake mkuu wa Klabu hio Sportpesa Tanzania kama sehemu ya fedha za mafanikio ya Ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC, Kombe la Shirikisho la Azam na kufanya vizuri ndani ya Mashindano ya CAF.
Ikumbukwe kuwa Klabu hio ilikuwa na Msimu mzuri 2022/23 kufuatia kufanikisha kutwaa mataji yote ya matatu ya soka Tanzania Bara Iikianza na Ngao ya Hisani, Ligi Kuu ya NBC na Kombe la Shirikisho, vivyo hivyo iliweza fika hadi ushiriki wa hatua ya Fainali ya Michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF).
#KoncepttvUpdates