Simba SC imethibitisha kumsajili tena aliyewahi kuwa beki wao David Kameta “alimaarufu kama Duchu” kwa Mkataba wa miaka mitatu.
Duchu alisajiliwa na Simba SC kwa mara ya kwanza 2020 akitokea Lipuli FC na alihudumu Simba SC kwa msimu mmoja tu kisha akatolewa katika vilabu vya Biashara United, Geita Gold na Mtibwa Sugar.
Kameta “Duchu” anakuwa mchezaji mpya wa nne kutambulishwa na atakuwa sehemu ya kikosi cha Simba SC kitakachosafiri kuelekea Uturuki Mei 11, 2023 kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.