Kupitia kurasa za mitandao ya kijamii ya Klabu ya Simba imeeleza kuwa itawatunuku vyeti maalum vijana wao mashujaa walioweza kufanikisha kufikisha kibegi cha jezi mpya za klabu hio juu ya kilele cha Mlima Kilimanjaro na kuifanya klabu hio kutimiza lengo lake.
Mashujaa hawa hapa Wametimiza lengo la klabu ya Simba kuzindua jezi kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro. Hivyo watajwa kustahili kutambuliwa kwa kazi kubwa waliyofanya ambapo katika siku ya #SimbaDay2023 wanatarajiwa kutunukiwa vyeti maalum.
“Mashujaa hawa hapa Wametimiza malengo la klabu ya kuzindua jezi kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro. Wanastahili kutambuliwa kwa kazi kubwa waliyofanya na katika hilo siku ya #SimbaDay2023 tutawakabidhi vyeti maalum. #NguvuMoja”____ Simba SC
#KoncepttvUpdates