Klabu ya Simba imemsajili Golikipa mahiri Jefferson Luis Teixeira Silva (@jefferson_luis01) kutokea nchini Brazil ukanda wa Amerika ya Kusini ili kulinda lango la klabu hio akichukua nafasi ya Golikipa Beno Kakolanya ambaye Simba SC iliweza achana naye baada ya mkataba wake kufikia kikomo huku Aishi Manula ambaye ni Golikipa nambari moja akiwa bado anapata ahueni ya kurejea uwanjani baada ya kufanyiwa upasuaji.
Luis ni miongoni mwa Walinda Lango Bora waliohusishwa sana kwenye tetesi za sajili za Simba kwa kipindi kirefu kwa dirisha hili kubwa la uhamisho wa wachezaji tangu kufunguliwa kwake rasmi.