Namungo FC kutokea Lindi, kusini mwa Tanzania imemtangaza aliyekuwa Kocha Msaidizi wa Yanga SC, Cedric Kaze kuwa Kocha Mkuu wa kikosi cha ‘Southern Killers’.
Kaze ameitumikia Yanga kwa misimu miwili tangu alipojiunga nayo mwaka juzi Oktoba 2020 na kwa kushirikiana na benchi la uufundi amefanikiwa kuisaidia timu hiyo kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC, Kombe Shirikisho la AZAM SPORTS na Ngao ya Jamii kwa misimu yote miwili.
#KonceptTvUpdates
