Azam Tv kupitia chaneli ya Sinema Zetu Channel no.103 wamezindua tamthilia zao mpya, tamthilia hizo ni Kazamoyo na Lolita.
Tamthilia mpya ya KAZAMOYO muandishi ni Dr Cheni inazungumzia juu ya visa,mikasa na maisha ya watu wa kijiji cha Kazamoyo
Tamthilia nyingine iliyozinduliwa ni ya Lolita muandishi wake akiwa ni William Mtitu ambayo inaelezea maisha ya Lolita aliyoyapita na kuleta kizaazaa.
Tamthilia hizi zinatarajiwa kuanza kurushwa na Azam Tv kupitia Channel ya Sinema zetu kuanzia 14.08.2023
Azam Tv tunapenda kuwapongeza sana waandaji wa tamthilia za Jeraha NA Fungu Langu kwa kutuheshimisha mmetufanya tupate hadhi inayostahili pia inawakaribisha wasanii mbalimbali kupeleka kazi zao
#KonceptTvUpdates