Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) imeujuza umma kuwa Serikali imefanya mabadiliko ya Viwango vya Utozaji kodi ya Majengo.
Viwango hivyo vimebadilika kufuatia SURA 289 kupitia Sheria ya Fedha ya 2023 ambapo viwango vya utozaji kodi hio umebadilika pamoja na wigo wa ukusanyaji kodi hiyo umeongezeka kwa kujumuisha nyumba zilizopo maeneo yote ya Wilaya.
Viwango hivyo vimebadilika kama ifuatavyo;
Nyumba ya Kawaida iliyokuwa inatozwa Shilingi 12,000/= kwa mwaka sasa itatozwa Shilingi 18,000/= kwa mwaka sawa na 1,500 kwa mwezi.
Nyumba za Ghorofa katika maeneo ya Majiji, Manispaa na Halmashauri za Miji zilizokuwa zinatozwa Shilingi 60,000/= kwa kila sakafu kwa mwaka sasa zitatozwa Shiringi 90,000/= kwa mwaka sawa na 7,500/=
Utekelezaji wa kutoza kodi hii ya majengo kwa kufuatwa mabadiliko mapya, unaanza mwezi Julai 2023.
Cc; TRA
#KonceptTvUpdates