Kikosi cha Wanajeshi wa Niger kimetangaza kumuondoa madarakani Rais wa Nchi hiyo, Mohamed Bazoum hivi karibuni kufuatia Kiongozi huyo kuzuiwa Ikulu na Kikosi cha Walinzi wa Rais kinachoongozwa na Jenerali Omar Tchiani.
Msemaji wa Jeshi hilo, Kanali Amadou Abdramane ametoa taarifa kupitia Televisheni ya Taifa akiwa na Wanajeshi wengine tisa, atoa sababu kuwa ni kuzorota kwa hali ya Usalama, Utawala Mbovu na Hali Mbaya ya Kiuchumi na Kijamii
Mipaka ya Nchi imefungwa na Amri ya Kutotoka Nje imetangazwa nchi nzima, pia huduma za Taasisi za Umma zimesitishwa hadi hapo taarifa nyingine itakapotolewa
Cc; Aljazeera
#KonceptTvUpdates