Simba SC ikiwa katika Siku za mwishoni kukamilisha ratiba yake ya kambi huko nchini Uturuki kuelekea Simba Day, Leo Alhamisi ya Julai 27 imecheza mechi yake ya pili ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya klabu ya Turan PFK.
Mechi hiyo imetamatika kwa upande wa Simba SC kuibuka na ushindi baada ya kuiangushia kichapo cha Mabao 2-0 Turan PFK.
Nyota wawili wa klabu ya Simba wamepata tikisa Nyavu za wapinzani hao na kuipa Simba Ushindi wa mabao hayo, ambapo Kibu Denis akiwa ametupia bao la kwanza na akafuatiwa na Fantastic Captain John Bocco kwa kuifungia bao la pili.
Mabao yote mawili yalipatikana katika Kipindi cha Pili cha mchezo huo baada ya Simba SC kutumia nafasi ya Makosa ya Wapinzani wao vizuri na kuwaadhibu.
#KonceptTvUpdates