Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo (@WizaraSanaa) Dkt. Pindi Chana ameshuhudia zoezi la utiaji Saini Mkataba wa makubaliano ya ukarabati wa Uwanja wa Benjamin Mkapa kati ya Wizara hio na Kampuni ya Beijing Construction Engineering Group (BCEG) ya China ambao utagharimu zaidi ya Sh. Bilioni 31 hadi kukamilika Julai 2024.
Uwanja wa Benjamini Mkapa umetengewa kiasi hicho cha bajeti ya fedha kufuatia changamoto zinazoukumba uwanja huo kwa kipindi kirefu.
Serikali kupitia wizara yenye dhamana hiyo imefanya hivyo kuhakikisha uwanja unakuwa na hadhi ya Viwango bora Barani Afrika pia kuweka nguvu ya kuhamasisha michezo nchini.
#KonceptTvUpdates