Uongozi wa Young Africans SC umethibitisha kuwa umefikia makubaliano na Klabu ya Azam FC kumnunua mchezaji wao Yannick Bangala.
Mchezaji huyo anakuwa wa Pili katika takwimu za Wachezaji wa Yanga kusajiliwa ndani ya Kikosi cha Wanalambalamba wa Chamazi Azam FC katika msimu huu wa Dirisha kubwa.
Ikumbukwe kuwa mchezaji wa kwanza kumalizana na Klabu ya Yanga ambaye alikuwa ndiyo wakwanza kusaini na Kuavalia Jezi ya Azam ni Feisal Salum (Fei Toto) baada tu ya kumaliza tofauti zilizojitokeza kwa takribani miezi Sita dhidi ya klabu yake hio ya zamani kabla ya kuuzwa.
Yannick Bangala anaondoka Yanga akiwa amewaacha Yanga katika nafasi nzuri ya Kusalia Bingwa Mtetezi wa Kombe la Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara alipokuwa chini ya Kocha Mkuu Professor Nabi na Msaidizi wake Cedric Kaze ambao wote wamekwisha achana na klabu hio na kenda kupata changamoto mpya katika majukumu yao mapya.
#KonceptTvUpdates