Biashara ya kununua mbegu za kiume imeshamiri katika Kaunti ya Murang’a nchini Kenya ambapo baadhi ya wanawake wanajitolea kulipa hadi Ksh 300,000 [TZS milioni 5.1] kuwalipa Wanaume wanaokubaliana nao ili wasababishiwe kushika mimba.
Wanaume ambao wanapendelewa zaidi katika biashara hii ni wale wenye umri kati ya miaka 20 hadi 40 na wanahitaji kuwa na sifa ambazo wanawake hao wanavutiwa nazo ikiwemo watu wenye akili na wengine hupendelea wanaume ambao ni warefu na wenye rangi ya ngozi ya wastani, yaani sio weupe sana wala weusi kupindukia.
Mmoja wa wanawake hao ameiambia gazeti la Taifa Leo kuwa wanawake wa siku hizi ambao wameamua kujitegemea kimaisha hawataki kuingia katika ndoa na badala yake wanatafuta tu mbegu ili waweze kuzaa na kulewa watoto wao.
“Hata hivyo, tunazingatia sana suala la kuwa na watoto wenye sura nzuri na pia akili nzuri ili waweze kufanya vizuri katika masomo,” amesema mwanamke huyo.
Cc; swahilitimes.co.tz
#KoncepttvUpdates