Rais wa Jmauhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt Samia Suluhu Hassan ameliagiza jeshi kujiandaa kabisa ili kuweza kukabiliana na Changamoto zitakazojitokeza kwenye Chaguzi zitakazofanyika Mwakani.
“Hatusemi tukafanye chaguzi za kutumia nguvu hapana, taratibu, sheria na miongozo ya uchaguzi itafuatwa lakini Jeshi na vikosi vyote vya ulinzi na usalama vikae tayari kukabiliana na hali yoyote itakayojitokeza, mwakani tunaenda kwenye uchaguzi mkuu na ule ndiyo wenye vishindo vikubwa basi ikabidi nitoe tu taarifa na kuwaweka ‘alert’ kwamba hayo mambo yanakwenda kutokea na jeshi hatuna budi kujiweka tayari,” – Rais @SuluhuSamia