Jurgen Klopp ameamua kuwa ataondoka Liverpool mwishoni mwa msimu huu.
Jurgen Klopp: “Niliiambia klabu tayari mnamo Novemba kwamba nitaondoka mwishoni mwa msimu”.
“Ninaishiwa na nguvu, huo ndio ukweli”.
“Ninapenda kila kitu kuhusu klabu hii na #LFC lakini najua kwamba siwezi kufanya kazi tena na tena na tena na tena”.
Pia, Sio tu Jurgen Klopp lakini inatarajiwa kuwa wasimamizi wasaidizi Pepijn Lijnders na Peter Krawietz na mkufunzi wa maendeleo Vitor Matos wataondoka Liverpool mwishoni mwa msimu.
Lijnders, ana nia ya kutafuta kazi yake mwenyewe katika usimamizi.
Mkurugenzi wa Liverpool, Jorg Schmadtke nae ataondoka katika klabu hiyo mwishoni mwa dirisha la usajili la Januari.( Cc; Fabrizio Romano)
Unahisi nani ata-fit nafasi ya Klopp Liverpool?
#KonceptTvUpdates